DIWANI ADAM SIMBAYA AGAWA UPENDO KWA WAJUMBE WDC MBALIZI ROAD



Diwani Kata ya Mbalizi Road Jijini Mbeya Mhe Adam Simbaya awashukuru  Wajumbe wa WDC Kata ya Mbalizi Road kwa ushirikiano mkubwa wanaotoa  katika Kata hiyo.

Hayo ameyaongea  katika Kikao cha WDC kilichofanyika  Matema Beach Wilayani Kyela na  kuwashukuru Wajumbe hao kwa  ushirikiano walioutoa kwa kipindi chote.


Pamoja na Kuwaaga Wenyeviti ambao  wanamaliza   muda wao,  Mhe Diwani alitoa zawadi  kwa wenyeviti wake wote wa Mitaa Minne kwa niaba ya WDC ikiwa ni  kumbukumbu yao kwa kipindi ambacho kimebakia kumalizia nafasi ya wenyeviti wa mitaa


Comments