FANYENI VIZURI MASOMONI MTUPE HESHIMA-KIKWETE
Maneno hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akihutubia wahutimu wa kidato cha Sita katika shule ya Kati ya Lugoba , Halmashauri ya Chalinze.
Ndg. Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa jimbo hilo aliwaasa wahitimu hao kuhakikisha wanafaulu ili waache deni la kufuatwa na wadogo zao wanaowafuata kwa upande mmoja, wawape heshima Walimu na wazazi pia kwa kufaulu vizuri.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mbunge kuzungumza na Wahitimu, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Sakasa aliishukuru serikali kwa kuendelea kupeleka pesa za Elimu bure , vifaa na kuongezeka kwa madarasa na walimu shuleni hapo huku akimuomba Mgeni rasmi kuendelea kuikumbuka shule hiyo kwa kuisaidia vifaa na kuongeza mabweni ya wanafunzi.
Comments
Post a Comment