TULIA TRUST YATOA MSAADA WA MABATI KWA MAMA MLEMAVU WILAYA YA MBEYA
Taasisi ya Tulia Trust leo tarehe 01/11/2022 imetoa msaada wa Mabati bando sita kwa Bi.Tabia Maarifa Mlemavu wa Miguu mkazi wa Kata ya Simambwe Halmashauri ya Mbeya DC wilaya ya Mbeya kwaajili ya kuezekea nyumba yake iliyokuwa inakabiliwa na changamoto ya mabati.
Akiongea kwa niaba ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Tulia Ackson Meneja wa Taasisi hiyo Jacklin Boaz amesema Dkt.Tulia aliguswa na maombi ya mama huyo ambaye ni mlemavu wa Miguu na siku ya leo wametekeleza maombi yake kwa kumpatia mabati .
Bi.Tabia Maarifa amewaomba wadau wengine kumsaidia kutokana na changamoto aliyonayo kwani inamlazimu kutoka Simambwe kwenda mpaka Mbeya Jiji kuombaomba kwa watu ili aweze kukizi mahitaji yake ya siku,amesema ombi lake ni kupatiwa mtaji wa kufungua duka ambao utaghalimu kiasi cha pesa za Kitanzania Tanzania Shilingi milioni mbili
Kwa upande wa Wananchi wamemshukuru Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Tulia Ackson kwa kugusa maisha ya watu wasiojiweza,ukizingatia jimbo hilo sio lake lakini ameweza kumsaidia mama Maarifa ambaye uwezo wake wa kutafuta ridhiki ni mpaka aombe misaada kwa watu barabarani.
Comments
Post a Comment