MADIWANI HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA WATEMBELEA VYANZO VYA MAJI



Na.Harubu Kabwe

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira MBEYA-WSSA tarehe 12/11/2022 ilitoa fursa kwa Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kutembelea vyanzo vya Maji ili kujionea namna umeme unavyokatika mara kwa mara na kuathiri huduma ya uzalishaji na usambazaji wa maji na Mamlaka kushindwa kuhudumia wateja na kushindwa kusukuma maji kutokana na kukatika kwa umeme kwenye mitambo hali inayopelekea kupungua uzalishaji kwa asilimia 30.


Changamoto nyingine iliyoelezwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa Mamlaka hiyo Injinia Barnaba Konga alisema kupungua kwa maji katika vyanzo kipindi cha kiangazi ni kutokana na kupungua kwa maji kwenye vyanzo vya mito na chemichemi na kupeleka kuwa na migao ya maji katika eneo la huduma.


Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mhe.Kefasi Mwasote kwa niaba ya Madiwani amesema watakwenda kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi baada ya kujionea hali halisi ya vyanzo vya maji na kuwaomba Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira MBEYA-WSSA waendelee kutoa elimu kwa kada mbalimbali.


Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Maji Prof. Aloys Mvuma amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuweka jicho kali kwenye swala la Maji.

Amesema amekuwa Mjumbe wa Bodi kwa kipindi cha miaka mitatu ametoa ushuhuda jinsi maji yanavyofikishwa kutoka kwenye chanzo hadi nyumbani baada ya kuwa mjumbe wa bodi kila tone la maji amekuwa analiheshimu baada ya kuona gharama kubwa zinazotumika kwa Mamlaka hiyo.


PICHA NA HAROUB TV

Comments