WAZIRI MKUI AMEANZA ZIARA YA SIKU MBILI MKOANI SINGIDA


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 05, 2022 ameanza ziara ya siku mbili mkoani Singida kwa kutembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Iglansoni kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Ujenzi wa kituo hicho ambao ujenzi wake umefikia asilimia 98 umegharimu shilingi milioni 500 na inategemea kuwahudumia wakazi 13608 wa vijiji vya Iglansoni na Mnyange kuanzia mwishoni mwa mwezi Agosti 2022.


Fedha hizo zitahusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Nje (OPD), Jengo la Maabara, na jengo la kichomea taka, jengo la upasuaji, jengo la wodi ya wazazi na jengo la kufulia

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kuendelea kutolewa fedha kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta zote ikiwemo afya, elimu, nishati na maji.

Comments