Uanzishwaji wa Benki ya Taifa ya Ushirika



Tume imeratibu uanzishwaji wa Benki ya Tafa ya Ushirika ambayo itamilikiwa
na Vyama vya Ushirika kwa asilimia 51 na taasisi na watu binafsi watamiliki
kwa asilimia 49. 

Lengo la kuanzishwa Benki hiyo ni kurahisisha upatikanaji wa
mitaji kwa wanachama. Benki hiyo inatarajiwa kuzinduliwa itakapokidhi kigezo cha kuwa na mtaji wa Shilingi Bilioni 15.

Hadi sasa benki hii mtaji wake umefikia Shilingi Bilioni 3.7. Tume inaendelea kuhamasisha Vyama vya
Ushirika na wadau wengine kununua hisa katika Benki hiyo.

Hayo yamebainishwa na Dkt. Benson O. Ndiege

Mrajisi wa  Vyama  vya Ushirika na Mtendaji  wa Tume Ushirika 




Comments