SIMBA DAY YAENDELEA KUINGIA DOSARI
Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania - TAS kwa pamoja na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu - LHRC tunalaani vikali kitendo kilichofanywa tarehe 8/8/2022 siku ya Simba Day cha kutumia jeneza, msalaba na kumtumia mtu mwenye Ualbino na kumfunga mikono kama msukule.
Hii ni kwenda kinyume na
haki za binadamu kwa kutweza thamani na utu wa mtu mwenye Ualbino.
Tunaamini kuna utani wa jadi katika michezo lakini isitumike hali ya mtu kamasababu ya kumuumiza na kuumiza wengine kwani kuna watu wengi ambao
tunajua wanahali hiyo na wanaumizwa na vitendo hivi vya kikatili.
Tunaiomba TFF isimamie jambo hili na Uongozi wa Simba uombe radhi kwa jamii ya watu wenye Ualbino na umma waWatanzania kwa kitendo hichi cha kinyama na kikatili na cha kibaguzi.
Comments
Post a Comment