RAIS SAMIA AWATAKA VIONGOZI KUWAHUDUMIA WANANCHI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
amesema Serikali imezuia kukata na kupandisha hadhi maeneo ya utawala kwa sababu yanaongeza gharama kwa Serikali.
Rais Samia amesema hayo leo wakati akihutubia wananchi wa Njombe
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba.
Aidha, Rais Samia amesema mwelekeo wa Serikali ni kunyanyua hali ya
uchumi wa nchi ili kuinua hali ya maisha ya mwananchi mmoja mmoja.
Rais Samia pia ametoa wito kwa Viongozi nchini kusimamia ipasavyo
miradi inayotekelezwa na Serikali ili kuwajengea fursa Watanzania
kufanya shughuli za maendeleo na kuinua kipato.
Vile vile, Rais Samia amewataka Viongozi wa Kata, Wilaya na Mikoa
kuhudumia wananchi na kutatua kero zao kwa kuzingatia utawala bora.
Comments
Post a Comment