RAIS SAMIA AFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYANI CHUNYA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na TAMISEMI kupitia
Halmashauri zote nchini na kuhakikisha zinaweka mipango ya kukusanya
mapato.
Rais Samia amesema hayo katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Chunya
Makongolosi kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 39 iliyofanyika
katika uwanja wa Matundasi.
Aidha, Rais Samia amesema mapato yanayokusanywa na Halmashauri
yakisimamiwa vizuri yanaweza kujenga miradi ya maendeleo kwa ajili ya
wananchi.
Akizungumza na wananchi wa Chunya mjini, Rais Samia ameagiza Madiwani na
Wenyeviti wa eneo hilo wanaopata mapato mengi kutokana na kutoa leseni nyingi za biashara kujenga kituo cha mabasi cha Chunya.
Vile vile, Rais Samia ameeleza barabara hiyo itafungua fursa za kibiashara kwa
wananchi wa Chunya kwani inaunganisha mkoa wa Mbeya na mikoa ya jirani.
Comments
Post a Comment