Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi awapongeza TPA
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Atupele Mwakibete amesema wananchi wa Mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mbeya sasa watapata huduma ya meli ya abiria baada ya Matengenezo ya meli Mv Mbeya II kukamilika.
Amezipongeza Mamlaka ya bandari (TPA),Shirika la bima la Taifa na Shirika la wakala wa meli nchini (TASAC ) kwa kuhakikisha meli ya Mv Mbeya II inaanza kufanya kazi.
"hivi ndiyo kumuunga mkono Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwa vitendo mipango yake ya kuijenga na kuiletea maendeleo nchi yetu kilichobakia sasa ni kufanya vikao na wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi ili kuboresha huduma na kutanua wigo wa kibiashara kimataifa" alisema Mwakibete
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi amewaagiza TASAC wakafanye ukaguzi kwenye meli za Ziwa Tanganyika maana zimekuwa zikikumbwa na ajari za mara kwamara .
Comments
Post a Comment