WAZAZI WEKEZENI ELIMU KWA VITENDO KWA VIJANA - MBUNGE BAHATI NDINGO




wamehimizwa kuwapeleka watoto wao kwenye taasisi za elimu zinazotoa elimu ya vitendo ili kuwajengea uwezo binafsi wa kujiajiri baada ya masomo.

Wosia huo ulitolewa na Mbunge wa Viti Maalumu, Bahati Ndingo kwenye mahafali ya wanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo.

Mahafali hayo yanafanyika kwa mara ya sita katika chuo hicho kwa wanafunzi wanaosoma kozi ya kilimo na mifugo.

Ndingo, alisema; "Nawaasa wazazi wahakikishe vijana wao wanapata elimu endelevu itakayowasaidia kufanya vizuri hata baada ya kumaliza masomo yao vyuoni. Uwekezaji wa elimu ulenge kuwapa uwezo binafsi wa kuwasaidia wengine pia kujikwamua kimaisha.," alisema

Mkuu wa Chuo cha Kaole, Sinani Simba, alisema; "Wanafunzi hawa wana ubobezi mzuri sana kwenye fani zao hizo mbili na wana weledi wa kutosha kutokana na mafunzo ambayo waliyoyapata hapa chuoni.," alisema na kuongeza kuwa;

"Wanafunzi wanaohitimu ni 122 kati ya hao 24 wanahitimu ngazi ya cheti (Certificate) ya kilimo na 33 diploma ya kilimo na 65 ni diploma ya uzalishaji wa mifugo.," alisema

Kwa hivi sasa chuo cha Kaole kinafundisha wanafunzi wanaohitimu cheti na diploma za kilimo na mifugo. Pia chuo kina wanafunzi waliothibitishwa na (National council for technical and vocational education training (NACTVET) wanaosoma masomo ya kilimo na mifugo.


Comments