Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson afanya kweli Shule za Sekondari
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini , Dkt. Tulia Ackson ametoa Madawati Kwa Shule za Sekondari Iduda,Tulia Ackson, na Itagano.
Tarehe 21/07/2022 Dkt.Tulia Ackson alianza ziara yake kwa kutembelea Shule ya Sekondari Iduda na kutoa Madawati 100 pamoja na Mabati 200
Tarehe 22/08/2022 Dkt.Tulia aliendelea na ziara yake kwa kutembelea shule ya Itagano pamoja na Tulia Ackson Sekondari School na kutoa mabati kwa kila Shule 200 pamoja na Madawati 100 kwaajili ya kuanza ujenzi wa kujenga hostel za wanafunzi wa shule hizo.
Akiongea kwa nyakati tofauti Tulia ameishukuru benki ya Nmb kwa kumuunga mkono katika kusaidia kufikia lengo la kuhakikisha kila shule katika jimbo la Mbeya Mjini inatatuliwa matatizo yake.
Comments
Post a Comment