MBUNGE MASACHE AZINDUA ZAHANATI YA GODIMA JIMBONI KWAKE


Mbunge wa Jimbo la Lupa wilayani Chunya Mkoani Mbeya Mhe. Masache Njelu Kasaka leo tarehe 20/07/2022 amezindua zahanati ya Godima iliyopo katika Kijiji cha Godima Kata ya Chokaa.

Zahanati hii imejengwa kwa Nguvu za wananchi pamoja na Serikali Kuu na kugharimu zaidi ya Tsh. million mia moja (100) .
Masache anaendelea na ziara zake kwa kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayoendelea kujengwa katika jimbo lake huku akiendelea kusikiliza kero na kuzitatua za wapiga kura wake pamoja na kutoa misaada mbalimbali jimboni humo.



Comments