KYELA A WABABE WA MASHINDANO YA MBEYA SUPER CUP 2022
Mashindano ya Mbeya Super Cup yamefika tamati tarehe 22/08/2022 katika wilaya ya Kyela mkoani Mbeya baada ya Timu ya Kyela A kuibuka Mabingwa Mashindano baada yakuifunga Timu ya Mbeya Dc goli moja kwa sifuli.
Kwa Upande wake Mgeni Rasmi wa Mashindano hayo.Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson amezipongeza Timu zote shiriki zikiwemo nchi ya jirani Zambia kushiriki Michuano hiyo licha ya kutofanya vyema Mashindano hayo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe.Juma Zuberi Homera amesema Timu Tatu ambazo zimefanya vyema zitakwenda kushiriki Mashindano ya Mbeya Season Samia Super Cup wilayani Mbarali timu hizo ni Kyela A ,Mbeya Dc,na Rungwe.
Mshindi wa Mbeya Super Cup 2022 amejichanyakulia Kombe pamoja na fedha Taslimu Tanzania shilingi milioni saba (7,000,000) pamoja na medali huku mshindi wa pili akijipatia fedha Taslimu Tanzania shillingi milioni tano (5,000,000) na medali na Mshindi wa Tatu akijipatia Tanzania Shilingi milioni tatu (3,000,000) na medali .
Comments
Post a Comment