HATI 100 ZAKABIDHIWAWA JIJI LA MBEYA


Ofisi ya ardhi Mkoa wa Mbeya imekabidhi hati mia moja za ardhi kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya zikihusisha maeneo ya wazi tisini na mbili,shule za msingi tatu,kiwanja cha mpira kimoja na masoko manne ili kukabiliana na uvamizi unaoweza kufanyika katika maeneo hayo.

Akipokea hati hizo kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Wakili Triphonia Kisiga amesema Halmashauri imeamua kuingia gharama ya kuyapima maeneo hayo ikiwa ni moja ya utekelezaji wa maagizo ya serikali kuyalinda maeneo hayo.


“Ndugu zangu wanahabari hii ni awamu ya kwanza tunaendelea kuyapima maeneo yetu yote ili tuyalinde dhidi ya uvamizi “ alielezea Wakili Kisiga.
Nawe msajiri msaidizi wa hati na nyaraka wa serikali Mkoa wa Mbeya ndugu Sadick Diombayo amesema kuwa serikali ina mkakati wa kuyapima maeneo yote inayoyamiliki ili yawe na hati na kuyalinda yasiweze kuvamiwa dhidi ya wavamizi wa ardhi.


Jiji la Mbeya ni miongoni mwa Majiji sita nchini ambapo limeanza kukua kwa kasi , ikiwa sehemu ya changamono iliyoikumba ni uvamizi wa viwanja kutokana na ongezeko la watu na makazi holela.

Vilevile Halmashauri ya Jiji la Mbeya kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wake Kisiga imeamua kuyapima maeneo yake ili kuyalinda yasivamiwe ambapo ofisi ya ardhi Mkoa inakamilisha zoezi hilo na kukabidhi hati miamoja.

Aidha Jiji la Mbeya linakuwa miongoni mwa Halmashauri za awali kuanza kutekeleza zoezi hilo huku baadhi ya Halmashauri hapa nchi zikikumbwa na uvamizi wa maeneo yao.

Comments