CHUNYA KUNUFAIKA NA MRADI WA USAMBAZAJI WA UMEME


Waziri wa Nishati Mhe.January Makamba,  amefanya ziara wilayani Chunya na kuhutubia wananchi wa kijiji cha Itumbi na kutoa Taarifa ifikapo mwezi disemba mwaka huu Vijiji vyote vitafikiwa na umeme.

Mradi wa  usambazaji umeme wilayani Chunya wenye gharama ya Tsh.Bil 9.2 unatekelezwa na kituo kikubwa cha kuongeza nguvu umeme(Substation) kinaenda kujengwa ili kumaliza tatizo la umeme wilayani Chunya.


Mbunge wa Jimbo la Chunya Masache Kasaka amemshukuru Waziri wa Madini  kwa kutembelea jimboni kwake na kuelezea namna wizara yake itakavyotatua changamoto za umeme

Comments