MAWAKILI WA SERIKALI, MAAFISA SHERIA KUTOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA ILI KUONGEZA WIGO WA UPATIKANAJI HUDUMA
Wizara ya Katiba na Sheria imeandaa Mpango utakaowawezesha Mawakili wa Serikali na Maafisa Sheria ambao ni Mawakili wa Kujitegemea au wana sifa za kuwa Mawakili wa Kujitegemea kuruhusiwa kutoa huduma za msaada wa kisheria hususani uwakilishi kwa mashauri ambayo hayana mgongano wa kimaslahi na mwajiri. Akifungua rasmi mafunzo ya Mawakili wa Serikali na Maafisa Sheria leo 28 Januari, 2026 jijini Arusha, Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA. Amos Makalla akimuwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera amesema kuwa Mpango huu utawawezesha Mawakili na Maafisa Sheria kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa jamii ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma, kuweka uendelevu wa huduma na kuimarisha ufanisi na utendaji katika kazi za sheria. Mh. Makalla amesema kuwa ni wajibu wa Mawakili wa Serikali kuhakikisha wanaongeza uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya haki na wajibu wao kwa lengo la kuendelea kujenga Taifa lenye amani na maendeleo. “Uhitaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa...