RIDHIWAN KIKWETE MGUU KWA MGUU KUTATUA KERO ZA ARDHI



Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete amezitembelea familia na makazi yenye migogoro ya ardhi ya muda mrefu kwa kuzifuata katika maeneo yao kwa lengo la kujionea uhalisia wa migogoro na kupata maelezo ya kina kabla ya kizitafutia ufumbuzi.



Naibu Waziri Kikwete amefanya hayo mkoani Morogoro jana tarehe 18 Agosti 2022 ambapo ametembelea baadhi ya maeneo na familia zenye migogoro ya muda mrefu ambapo miongoni mwao ametembelea familia ya Bwana Felician Bupiripiri na Bwana Rajabu Kyara ambao wamekuwa wakigombea kiwanja namba 1 na namba 3 vilivyopo mtaa wa Boma Road katikati ya mji wa Morogoro.
Katika hali isiyo ya kawaida Naibu Waziri Kikwete alifika katika nyumba hiyo na kumkuta Bibi Neli Lukwaja ambaye ni mke wa Bwana Felician Bupiripiri na kutembeza maeneo yote ya nyumba hiyo ambayo wamekuwa wakiimiliki kwa muda mrefu huku akilalamika kutotendewa haki na Rajabu Kyara ambaye nae anadai kumilikishwa kwa hati.

Comments